
Waataalamu wa afya wameitaja wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu kuwa inakabiliwa na tatizo la utapiamlo mkali kwa watoto wadogo, kutokana na lishe duni dhidi yao.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya halmashauri ya mji wa Bariadi, Dkt. Rosemary Mushi, ameyasema hayo wakati akipokea msaada mbalimbali ya kibinadamu iliyotolewa na watumishi wanawake wanaohudumu idara ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) mkoa wa Simiyu.