
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amewakaribisha wawekezaji kutoka katika maeneo mbalimbali duniani kuja kuwekeza kwenye kilimo na kuahidi kuwa serikali itatoa ardhi na kuweka mazingira bora.
Bashe ametoa kauli hiyo ya ukaribisho Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na washiriki wa uzinduzi wa Jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika (AGRF), uliofaywa na Rais Samia Suluhu Hassan.