
Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP. Justine Masejo amesema wamekamata jumla ya watuhumiwa 11 wakiwa na mirungi bunda 528 zenye uzito wa zaidi ya kilogramu 162 ambayo walikuwa wakiisafirisha kwa kutumia gari na pikipiki.
Katika hatua nyingine Polisi mkoani humo kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imemfikisha mahakamani mtu mmoja aitwaye Julius Raphael Mollel (27) mkazi wa kijiji cha Lashaine wilaya ya Monduli kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili (08) ambaye jina lake limehifadhiwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa hilo.