
Watu saba kutoka kaya nne tofauti wamefariki baada ya kula nyama ya samaki aina ya Kasa anayesadikiwa kuwa na sumu. Kaimu kamanda wa polisi mkoani Rufiji, Canute Msacky amesema tukio hilo limetokea katika kijiji cha bweni na kijiji cha Kanga, kara ya kanga, wilaya ya Mafia.
Watu hao walifariki majira tofauti tofauti na miili yao imefanyiwa uchunguzi wa kitabibu katika hospitali ya wilaya Mafia na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.