
Mamlaka ya bandari ya Madagascar imesema watu 22 wamefariki dunia wakati mashua iliyokuwa imewabeba kutoka Madagascar imepinduka walipokuwa wakisafiri kuelekea kisiwa cha Ufaransa cha Mayotte.
Mamlaka ya bahari na mito imesema Boti hiyo ilikuwa imebeba watu 47, imepinduka katika bahari ya kaskazini mwa Madagascar.