
Watoto wawili wa kitongoji cha Malangi mtaa wa Malangi wilaya ya Babati mkoani Manyara wamefariki dunia mara baada ya kusombwa na maji katika korongo la changarawe wakiwa wanatoka shule kuelekea nyumbani.
Watoto hao ambao ni wanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi kiongozi wamefariki dunia mara baada ya kushindwa kuvuka korongo lililojaa maji yalitokana na mvua kubwa iliyonyesha kwa lisaa limoja na nusu na kuchumuliwa na maji hayo.
Wazazi wa watoto hao pamoja na majirani wameiomba serikali kujenga shule katika eneo hilo kwani watoto wao hutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu kwani hukutana na wanyama wakali pamoja na kushindwa kuvuka makorongo pindi waendspo shule hasa kipindi hiki cha mvua.