fbpx

Wakazi mkoani Mara kuingiliwa kimwili usiku

Katika hali isiyo ya kawaida, wakazi wa Kijiji cha Myamswa wilayani Bunda mkoani Mara wamepatwa na taharuki baada ya kuibuka kwa tatizo la kuingiliwa kimwili usiku na watu wasiofahamika kwa jinsia zote huku hali hiyo ikihusishwa na imani za kishirikina.

Wakizungumza na Jambo FM, baadhi ya wakazi wa Kijiji hicho wamesema tatizo hilo lipo kijijini hapo ambapo wamekuwa wakiingiliwa kimwili hasa nyakati za usiku wakiwa walelala na kuwa jambo hilo linatendeka kwa jisnia zote Pamoja na watoto, hali ambayo imezua taharuki kijijini hapo.

Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho amebainisha namna mtu huyo anayeingilia watu wa kinsia ya kishirikina anavyofanya vitendo hivyo hadi kwa watoto hasa wasichana

“Ana dawa ile ya kunuia yaani watoto wanakuja kama ndege wakirundikana pale kwake akiwa ameandaa miwa kuwapa wanafunzi anafanya nao tendo hilo, kwa siku anaweza kufanya na wanafunzi zaidi ya watano hadi kumi, anafanya na mmoja baada ya mwingine”

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights