
Wakandarasi wazawa wanaotekeleza miradi ya ujenzi wa barabara mkoani Ruvuma, wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na serikali yake ya awamu ya sita lwa kuwaamini na kuwapatia miradi mingi iliyowajengea uwezo zaidi na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Mkurugenzi wa kampuni ya Ovans Construction Ltd, Valence Urio amesema katika kipindi cha miaka miwili cha Rais Dkt. Samia kumekuwa na mafanikio makubwa kwai miradi mingi ya barabara za vijijini na mijini zimetekelezwa na wakandarasi wazawa hali ambayo imewasaidia kupata kipato cha kuhudumia familia na kuchangia maendeleo ya mkoa huo.