fbpx

Wafungwa 66 wafariki ndani ya miezi miwili Kongo

Wafungwa 66 wamefariki tangu Januari mwaka huu huko Makala, gereza kuu katika mji mkuu wa DRC, Kinshasa, kwa sababu ya mazingira ambamo wanazuiliwa, kulingana na kiongozi wa shirika moja la haki za binadamu nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Wafungwa hao walifariki kwa utapiamlo, kukosa hewa, au kukosa huduma, Wafungwa wawili wapya ambao walifariki kutokana na mazingira ambamo walikuwa wanazuiliwa, wanafikisha idadi ya vifo kufikia 35 kwa mwezi wa Februari pekee.

Mnamo mwezi Januari, watu 31 walifariki ikiwa ni pamoja na mwanamke mmoja katika jela la Makala.

Jela hiyo ambayo ilijengwa wakati wa enzi za ukoloni kwa uwezo wa kupokea watu 1,500, kwa sasa lina wafungwa 10,790, wakiwemo 7,780 walio katika kizuizi cha muda.

Tangu mwanzoni mwa mwaka, mamlaka ya mahakama imeruhusu kuachiliwa kwa masharti kwa wafungwa 635 ili kupunguza idadi ya wafungwa katika jela.

Rais  Tshisekedi amesema ameweka ulinzi na uendelezaji wa haki za binadamu na uhuru wa kimsingi miongoni mwa vipaumbele vya mamlaka yake na serikali ya jamhuri.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights