
Wafanyakazi wanne wa halmashauri ya Shinyanga wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Shinyanga kwa tuhuma ya kumdanganya muajiri kunufaika kwa watu 22 kwenye mfuko wa afya ya jamii CHF kwa thamani ya shilingi milioni 8.
Waliofikishwa katika mahakama hiyo ni Stella Thomas, katibu wa afya, Ferdinard Mazani, Mhasibu, wengine ni Saimon Katamba, muweka hazina, pamoja na Josephat Rapahael, mhasibu msaidizi.
Watuhumiwa hao wamekana makosa yao mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa Mh. Yuphi Zahoro na kesi hiyo itasomwa kwa hoja za awali tarehe 4,4,2023.