
Wachezaji wawili wa mpira wa miguu wamefariki dunia jumamosi marchi 11 baada ya kupigwa na radi wakati mchezo wa kirafiki kati ya timu ya Manyansi FC dhidi ya Gianchore FC katika uwanja wa Manyasi uliopo kaunti ya Kisii nchini Kenya.
Mwenyekiti wa shirikisho la soka la kaskazini la Kitutu Chache, Evans Akanga amesema wachezaji hao walipigwa radi na kufariki papo hapo wakati wa mchezo huo wa kirafiki.