fbpx

Vumbi kutoka jangwa la Sahara kuathiri nusu ya Cameroon

Waziri wa uchukuzi wa Cameroon amesema kwamba kiwango kikubwa cha vumbi kutoka jangwa la sahara kinatarajiwa kuathiri nusu ya Cameroon.

Waziri Ernest Ngalle Bibehe, ameonya kwamba vumbi hilo linaweza kusababisha ajali za barabarani kutokana na kupunguza uwezo wa madereva kuona mbali. Taarifa ya waziri huyo imeonya kwamba vumbi hilo linaweza pia kusababisha matatizo ya kupumua.

Vumbi kubwa linaloshuhudiwa kwa sasa katika eneo la kaskazini mwa Cameroon na huenda likaathiri maeneo manne ya nchi hiyo katika siku za hivi karibuni. Tahadhari imetolewa ikiwataka watu kuendesha magari kwa makini na kufunika macho pamoja na pua.

Cameroon hushuhudia kiwango kikubwa cha vumbi kutoka jangwa la Sahara kila mwaka, hasa sehemu za kaskazini na kusini.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights