
Wananchi wanaotakiwa kuhama katika vijiji vya vitatu vya Serengeti, Tamu na Nyatwali, vilivyopo katika kata ya Nyatwali wilayani Bunda, ili kupisha shughuli za uhifadhi za hifadhi ya taifa ya Serengeti, wamesema fidia wanayopewa na serikali ni ndogo ikilinganishwa na maisha wanayotarajia kwenda kuishi huko watakapohamia.