
Idadi ya vifo vilivyotokana na kimbunga Freddy nchini Malawi na Msumbiji imeongezeka na kuvuka watu 200 baada ya kimbunga hicho kuvunja rekodi na kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi wakati kilipopiga kwa mara ya pili huko afrika katika kipindi cha chini ya wiki tatu.
Wafanyakazi wa uokoaji wameonya kuwa huenda wakawepo waathirika zaidi wakati wakiendelea na msako katika vitongoji vilivyoharibiwa, kuwatafuta manusura hata pale matumanini yalipopungua.