
Wizara ya utamaduni, sanaa na michezo imeanza kutekeleza maagizo ya waziri mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) ya kuanza ukarabati wa uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa ziara ya kujipanga kutekeleza maagizo hayo, machi 5, 2023 katibu mkuu wa wizara hiyo. Saidi Yakubu amesema ukarabati huo utaanza mara baada ya mshauri mwelekezi kukamilisha kazi yake.
Ukarabati huo utafanyika kwa awamu tatu.