fbpx

Uteuzi wa Manaibu Waziri waibua mjadala Kenya

Rais William Ruto mnamo amewateua mawaziri wasaidizi 50 ambao wamepewa kusimamia wizara 22 ambapo kwenye orodha hiyo iliyotangazwa kupitia taarifa ya mkuu wa utumishi wa umma, Felix Koskei, idadi kubwa ya wateuzi hao ni wanasiasa wa muungano wa chama tawala Kenya kwanza walioshindwa kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Uteuzi huo wa mawaziri wasaidizi 50 wa Wizara 22 walioidhinishwa na tume ya utumishi wa umma, umepokelewa kwa hisia tofauti  na wa Kenya.

Wengi katika mitandao ya kijamii wamehoji utashi wa Rais Ruto wa kutimiza ahadi yake wakati wa kampeni mwaka jana ambapo aliahidi kuwa serikali yake itajumuisha kwa kiasi kikubwa wananchi wa tabaka la chini aliowaita ‘mama mboga na boda boda’.

Serikali imekosolewa pia kwa kufeli kupunguza mzigo wa kuajiri maafisa wengi serikalini wanaolipwa fedha nyingi za walipa ushuru, wakati ambapo uchumi wa Kenya unasuasua na wakenya wengi wakilalamikia ugumu wa maisha.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights