
Mataifa ya Urusi, China na Iran yameanza mazoezi ya kijeshi katika bahari ya Arabia yanayotajwa kuwa ni mkakati wa Urusi kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kijeshi na China pamoja Iran.
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema katika taarifa yake kuwa mazoezi hayo ya pande tatu yaliyopewa jina la ‘Usalama wa Majini 2023’ yameanzia katika eneo la Bahari ya Chabahar nchini Iran yakihusisha silaha mbalimbali.