fbpx

Urusi yakataa hati ya ICC ya kumkamata Putin

Serikali ya Urusi imejibu agizo la kukamatwa kwa Rais wa Urusi, Vladmir Putin ikisema kuwa maamuzi ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, ICC hayana maana yoyote kwa nchi yao.

Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema nchi ya Urusi sio mwanachama kwenye mahakama ya ICC na wala haina wajibu wowote chini yake.

Urusi imesema maafisa wa Urusi wamelichukulia agizo la kukamatwa kwa Rais Putin na kamishna wa haki za watoto wa Urusi, Maria Alekseevna Lvova-Belova sawa na vikwazo vingine vinavyoikabili Urusi kutoka mataifa ya magharibi.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights