fbpx

Umoja wa Ulaya kutanua uwekezaji nchini Kenya

Umoja wa Ulaya umesema utatanua uwekezaji wake nchini Kenya kwa mamilioni ya dola ukilenga kuimarisha mahusiano na taifa hilo la Afrika mashariki katikati mwa ushindani kutoka China.

Akizungumza katika siku ya kwanza ya jukwaa la biashara kati ya Kenya na umoja wa Ulaya mjini Nairobi, balozi wa umoja wa Ulaya nchini Kenya, Henriette Geiger, amesema uwekezaji huo utazilenga sekta ambazo bado hazijaimarishwa.

Geiger amesema mikataba mipya itakayotiwa saini ni sehemu ya mkakati wa umoja wa Ulaya wa kukusanya kiasi dola bilioni 340 kusaidia sekta ya miundombinu ya umma na binafsi kote ulimwenguni ifikapo mwaka 2027. Miongoni mwa makubaliano yatakayofikiwa ni pamoja ni ahadi ya mchango wa dola milioni 200 kuisaidia benki ya biashara na maendeleo inayoendeshwa kwa pamoja na mataifa kadhaa ya Afrika.

Benki hiyo imekuwa ikizisaidia kampuni za mataifa ya mashariki na kusini mwa Afrika zilizoathirika na vita nchini Ukraine

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights