
Ukraine imekanusha kuhusika kwa namna yoyote na shambulio lililotokea mwezi Septemba mwaka jana kwenye mabomba ya Nord Stream, ambayo yalibeba gesi ya Urusi kwenda Ulaya.
Ufafanuzi wa Ukraine unakuja baada ya ripoti ya gazeti la New York Times, ambayo inawataja maafisa wa kijasusi wa Marekani ambao wanasema kundi linalounga mkono Ukraine ndilo linalaumiwa.
Katika ripoti tofauti, vyombo vya habari vya Ujerumani vinasema wachunguzi wanaamini walitambua mashua iliyotumiwa kutega vilipuzi ambapo safirishaji wa gesi kupitia bomba ulikuwa umesitishwa kabla ya milipuko hiyo.