fbpx

Uhalifu: Polisi yakamata bastola kwa wahalifu

Jeshi la Polisi mkoani Arusha, limefanikiwa kukamata bastola moja aina ya CZ 75 LUGER yenye namba za usajili A487385 pamoja na risasi 71 za bastola, iliyokuwa inatumiwa na wahalifu.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Justine Masejo, amesema silaha hiyo pamoja na risasi, zilipatikana katika nyumba iliyopo huko maeneo ya Ilkyurei, Kata ya Kiranyi, wilaya ya Arumeru na mkoa wa Arusha.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights