
Serikali imetoa taarifa ya uwepo wa ugonjwa ambao bado haujajulikana mkoani Kagera katika Wilaya ya Bukoba Vijijini, Kata ya Maruku na Kanyangereko, Vijiji vya Bulinda na Butayaibega ambapo watu watano wamefariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Serikali, Prof Tumaini Nagu amebainisha jumla ya watu saba wanasadikika kupata dalili za homa, kutapika, kutokwa damu maeneo mbalimbali ya mwili na figo kushindwa kufanya kazi.