fbpx

Uganda yaweka mipango ya sheria mpya dhidi ya mashoga

Spika wa bunge la Uganda, Anita Among amekosoa tabia ya madola ya magharibi ya kutoheshimu tamaduni za watu wengine na badala yake kung’ang’ania misimamo yao kama uozo wa ushoga na ubaradhuli.

Spika wa bunge la Uganda, Anita Among amesema hayo katika ujumbe aliotuma  kwenye mtandao wa kijamii wa twitter na kusitiza kuwa, nchi hiyo ya Afrika Mashariki katu haitaunga mkono vitendo vichafu vya mapenzi ya watu wa jinsia moja.

Amebainisha kuwa, bunge la Uganda kuanzia leo machi mosi litaanza kujadili muswada wa marekebisho ya sheria ya kupambana na ushoga na kueleza kuwa, lengo la sheria hiyo ni kuwalinda waganda dhidi ya fitina ya mashoga na waungaji mko wao.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda wiki iliyopita, alisisitiza kwa mara nyingine tena kwamba, nchi yake haitaunga mkono vitendo hivyo vichafu vya mapenzi ya watu wenye jinsia moja.

Alisema kuwa, nchi za magharibi zinapaswa kuacha kutwishana misimamo na mitazamo yao; na kulazimisha nchi zinazopinga kukumbatia vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na maadili.

Kadhalika mwezi uliopita, maaskofu na viongozi wengine wa kanisa la kianglikana barani afrika wakiwemo wa uganda, walitishia kujitenga na kanisa la uingereza kwa kubariki na kuruhusu ndoa na mahusiano ya watu wenye jinsia moja

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights