
Wanaume sita wamekamatwa nchini Uganda kwa kujihusisha na ‘mapenzi ya jinsia moja’, msemaji wa polisi ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Ijumaa, siku moja baada ya Rais Yoweri Museveni kutangaza watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja kuwa wamepotoka.
Msemaji wa polisi, James Mubi amesema kupitia mtandao wa kijasusi kuwa wamewakamata wanaume hao sita kwa kufanya mapenzi ya jinsia moja katika chumba kimoja huko Jinja mji ulio umbali wa kilomita 80 mashariki mwa mji mkuu wa Kampala.