fbpx

Uchumi wa Nigeria waleta hali mbaya kwa raia

Raia wa Nigeria wanakabiliwa na hali mbaya zaidi ya kiuchumi, siku chache kabla ya uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika jumamosi katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika.

Kuimarika kwa uchumi wa nchi hiyo inayoozungumza kiingereza, nchi yenye wakazi milioni 215, 63% ambao ni maskini, itakuwa moja ya masuala makuu ya uchaguzi, pamoja na ukosefu wa usalama uasi wa kijihadi, uhalifu, madai ya watu wanaotaka kujitenga.

Nigeria ina maliasili nyingi, hasa katika hidrokaboni, lakini janga la uviko-19 na kuzuka kwa vita nchini Ukraine vimesababisha uchumi wake kudorora, na ambao tayari umeathiriwa na ghasia ambazo zinazoofisha kilimo na biashara katika sehemu kubwa za nchi. Mfumuko wa bei unakaribia 22%, na sarafu ya kitaifa, naira, inaendelea kupoteza thamani dhidi ya dola ambapo kwa sasa naira 750 inauzwa dola moja , dhidi ya naira 200 mwaka wa 2015.

Katika muktadha huo, ikiongezwa kwa mlipuko wa bei ya petroli, ambayo imeongezeka karibu mara mbili naira 330 kwa lita dhidi ya 165 miezi michache iliyopita.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights