
Wananchi wa Tunisia wamechoma moto bendera ya Marekani katika maandamano yao ya kuwaunga mkono watu wa Syria na kupinga vikwazo vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya nchi hiyo.
Maandamano hayo yaliyofanyika kwa ajili ya kuwatetea watu wanaodhulumiwa wa Syria na kupinga uvamizi na vikwazo vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya nchi hiyo, waandamanaji hao walichoma moto bendera ya Marekani na kulaani sera za kibeberu za nchi hiyo.
Wananchi wa Tunisia pia wameeleza mshikamano wao na taifa la Syria, hasa kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibunii nchini humo na kuua maelfu ya watu.