
Rais wa Tunisia, Kais Saied amemteua Kamal Feki kuwa waziri wake mpya wa mambo ya ndani, saa chache baada ya Taoufik Charfeddine kujiuzulu wadhifa huo huku kukiwa na msako mkali dhidi ya viongozi mashuhuri wa upinzani.
Saied alitoa amri mbili siku ya Ijumaa, ya kwanza ya kumuondoa Charfeddine na ya pili kumteua Feki, gavana wa zamani wa Tunisia, kama mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, ofisi ya Rais ilisema katika taarifa kwa vyombo vya habari.