
Mamlaka ya vifaa tiba nchini (TMDA) imewataka watumishi katika sekta ya afya kuwa makini na matumizi ya vifaa tiba na vitendanishi ambavyo havina ubora kwani vinaweza kuleta madhara kwa binadamu huku ikiwataka kutolea taarifa kwa uwepo wa vitendansishi hivyo kwa mamalaka hiyo ili viweze kuchukuliwa hatua.
Katika kukabiliana na changamoto ya vifaa tiba na vitendanishi ambavyo vimekuwa vikileta madhara kwa wagonjwa mamlaka ya vifaa tiba tmda imekuja na mpango wa kukabiliana na tatizo kwa kutoa elimu kwa wataalamu wa afya.
Christian kapinga ambeye ni afisa usajili wa dawa mamlaka ya dawa na vifaa tiba Tanzania akaeleza namna wanavyochukua hatua kuzuia bidhaa feki kuingia nchini.
Wauguzi pamoja na watalam kutoka idara ya afya wamesema mafunzo hayo yatasaidia kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo katika utoaji wa huduma.