fbpx

Takwimu: watanzania 620,000 wana ulemavu wa macho

Bi. Ziada Sellah

Inakadiriwa kuwa watanzania takribani 620,000 wana ulemavu wa macho nchini ikiwa ni sawa na asilimia moja ya watu kwenye nchi zinazoendelea na za uchumi wa kati kwa mujibu wa makadirio na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO).

Hayo yamesemwa  na Bi. Ziada Sellah kwa niaba ya Katibu mkuu wa wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe katika uzinduzi wa miradi ya Afya ya macho yenye jumla ya thamani ya Tsh. Bilioni 1.47 inayofadhiliwa na shirika la Christoffel Blinden Mission (CBM) uliofanyika katika Ofisi za WIzara ya Afya jijini Dodoma.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights