
Watalii jijini Paris wameshangazwa kuona jiji hilo lilivyo chafu na lina harufu mbaya kutokana na taka ambazo hazijakusanywa kwa sababu ya mgomo wa wakusanya taka katika mji huo, dhidi ya serikali kuongeza umri wa kustaafu na kupandisha kiwango cha michango ya pensheni kamili.
Takriban tani 6,600 za takataka zimerundikwa kando ya barabara kuu kwa wiki nzima sasa, mamlaka imesema.