
Leo tarehe 17 Machi Taifa la Tanzania linaadhimisha miaka miwili toka aondoke aliekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano hayati John Pombe Magufuli aliyedumu katika nafasi ya urais kuanzia mwaka 2015 hadi kifo chake mwaka 2021. Akiwa Rais wa kwanza nchini kupoteza maisha akiwa madarakani.
Pia aliwahi kuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuanzia mwaka 2000 hadi 2005 na 2010 hadi 2015 na alikuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika kuanzia 2019 hadi 2020.