
Wataalamu kutoka taasisi ya kimataifa ya Moody’s inayojihusisha kuzifanyia tathimini nchi mbalimbali dunia ili kujua uwezo wao wa kukopesheka katika masoko ya fedha ya kimataifa, wamewasili nchini kwa ajili ya kuifanya tathimini nchi ya Tanzania.
Waziri wa fedha na mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema tathimini hiyo ni fursa kwa Tanzania kuweza kuyafikia masoko ya fedha ya kimataifa yatakayoiwezesha nchi kupata rasilimali fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi.