fbpx

Stand united kuikabili Mwadui FC kwenye First League

Ligi daraja la pili maarufu kama First League itaendelea hii leo kwa michezo miwili kutoka kila kundi ambapo kundi B stand united kutoka Shinyanga baada ya kupoteza mchezo uliopita ugenini leo itakuwa mwenyeji wa Mwadui FC katika uwanja wa Mwadui Complex majira ya saa 10 jioni huku Mbao FC ikiialika Alliance katika uwanja wa CCM Kirumba ikiwa ni dabi ya jiji la Mwanza.

Kunako kundi A Tunduru korosho inacheza na majimaji katika dimba la majaliwa mkoani lindi huku TRA FC itaialika cosmopolitan katika uwanja wa majengo Complex mkoani Kilimanjaro.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights