
Kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu soka Tanzania bara February 27 mwaka huu dhidi ya wakata miwa wa Mtibwa Sukari timu ya Singida Big Stars ya mkoani Singida imesaini mkataba mpya wa udhamini na kampuni ya uuzaji wa mafuta nchini, Nassco Limited.
Udhamini huo ni wa kuwajazia mafuta kwenye basi la timu hiyo mpaka juni 2024, na hivyo mkataba umeanza punde kumalizia kipindi chote cha msimu uliobaki na utaendelea hadi msimu wote ujao wa ligi kuu ya NBC msimu wa mwaka 2023/24.
Mkataba huo umesainiwa na mtendaji mkuu, John Kadutu na mwakilishi wa kampuni hiyo katika ofisi za Nassco Ltd.