
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya bodi ya Ligi Kuu Tanzania bara imeitoza klabu ya Singida Big Stars faini ya Tsh milioni 1.
Hii ni kwa kosa la kukataa kuingia kwenye chumba maalum cha kuvalia kabla na wakati wa mchezo wake na Simba SC uliomalizika kwa ushindi wa magoli 3-1 kwa wenyeji Simba SC katika dimba la Benjamin Mkapa jambo lililowalazimu maafisa wa mchezo huo kuikagua timu hiyo katika eneo lisilo rasmi.
Katika hatua hatua nyingine rungu la adhabu limemwangukia kocha wa timu ya Dodoma Jiji, Melis Medo amefungiwa michezo 3 na faini ya shilingi milloni 1 kwa kosa la kumpokonya kadi mwamuzi wa mchezo kati ya Dodoma na Mtibwa Sukari na kumuonesha mwamuzi wa akiba ambae pia aliondolewa katika eneo la ufundi kwa kuneshwa kadi nyekundu.