
Jeshi la Polisi nchini Somalia limesema takriban watu watano wameuawa na wengine 11 kujeruhiwa, akiwemo Gavana Gedo AHMED BULLE GARED, katika shambulio la kujitoa mhanga lililotokea kusini magharibi mwa nchi hiyo.
Shambulio hilo, japo hakuna kundi lililojitokeza kudai kuhusika lakini linahisiwa kutelekezwa na wanamgambo wa Al Shabab, wenye mfungamano na Al-Qaeda na ambao mara kwa mara hufanya mashambulizi ya kujitoa mhanga katika nchi hiyo isiyo na utulivu.