
Serikali nchini imewataka Wachimbaji wa Madini kuzingatia Kanuni za Usalama na kufuata sheria na taratibu za Uchimbaji ili kuepusha ajali katika maeneo ya uchimbaji.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa Machi 17, 2023 alipotembelea eneo la ajali ya wachimbaji wadogo waliofunikwa na kifusi na kufariki la Igando Kata ya Magenge, Tarafa ya Butundwe mkoani Geita machi 10, 2023.