fbpx

Serikali yatoa bilioni 2.2 kuboresha makumbusho ya taifa

Mhe. Mary Masanja, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii

Serikali kupitia Mpango wa Fedha za Maendeleo ya Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19 imetoa Sh2.2 bilioni kwa ajili ya kuboresha na kukarabati maeneo mbalimbali ya kihistoria ikiwamo Makumbusho za Taifa na malikale kwa lengo la kuendelea kuvutia watalii wanaokuja nchini.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja ameyasema hayo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilipokagua marekebisho na ukarabati wa makumbusho ya azimio la Arusha na makumbusho ya elimu ya viumbe jijini Arusha.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights