
Serikali imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 4.6 kwa ajili ya kufanya maboresho makubwa katika ranchi ya Kongwa ikiwa ni pamoja na ununuzi wa mbegu bora za ng’ombe, uchimbaji wa visima na ununuzi wa matrekta.
Meneja wa Ranchi ya Kongwa, Elisa Binamungu amebainisha hayo wakati akisoma taarifa ya utendaji wa shamba la mifugo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua shamba la mifugo la Narco – Kongwa ili kujionea maendeleo ya shamba na shughuli za ufugaji.