
Serikali imepanga kujenga nyumba 300 kwa ajili ya watumishi wa umma kutoka kada mbalimbali, kwa mwaka ujao wa fedha 2023/2024.
Hayo yamebainishwa na Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Deogratias Ndejembi, alipotoa taarifa kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge TAMISEMI, iliyozuru wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.