
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassani amekutana na mwenyeji wake Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa na kufanya nae mazungumzo jijini Pretoria hii leo Machi 16, 2023.
Rais Samia aliwasili jijini Pretoria nchini Afrika ya kusini hapo jana Machi 15,2023, kwa ajili ya ziara ya kiserikali ya siku moja akiwa ameambatana na ujumbe wake.