
Cristiano Ronaldo amelipwa USD 334,637 kama fidia ya gharama za kisheria alizotumia wakati akijitetea katika kesi ya madai ya kumbaka mwanamke katika chumba cha hoteli jijini Las Vegas, Marekani mwaka 2009.
Kesi hiyo ilitupiliwa mbali June 2022 baada ya hakimu kuona kwamba wakili wa mlalamikaji alijihusisha na utovu wa nidhamu kiasi kwamba isingewezekana kwa Ronaldo kuwa na kesi ya haki. Jaji Jennifer Dorsey alitoa uamuzi wa wakili anayemwakilisha mlalamikaji Kathryn Mayorga, Leslie Stovall kumlipa Ronaldo $334,637.50 baada ya wakili huyo kuhukumiwa kwa kumdhuru mwanasoka huyo kupitia uwakili wa imani potofu.
Hapo awali iliwahi kuripotiwa kuwa mlalamikaji Kathryn Mayorga alinukuliwa akisema alilazimishwa kusaini makubaliano ya kutofichua ukweli na kulipwa $375,000 kufuatia madai hayo ya ubakaji ambayo hata hivyo Ronaldo alisisitiza kuwa yeye na mwanamke huyo walikutana kwa ridhaa yake