
Rais wa Kenya William Ruto amemuonya Raila Odinga dhidi ya kufanya maandamano kinyume cha sheria yatakayosababisha uharibifu wa maisha ya watu na mali pamoja shughuli za biashara nchini Kenya.
Katika kujibu vitisho vya Odinga na viongozi wengine wa upinzani kuongoza maandamano ya nchi nzima wiki ijayo, Rais Ruto ameongeza kuwa Kenya ni nchi inayoongozwa kwa sheria na hakuna aliye juu ya sheria.