
Shinikizo kwa soka la Canada limesababisha kujiuzulu kwa Rais wa shirikisho hilo Nick Bontis jana jumatatu.
Nick Bontis amejiuzulu kama Rais wa soka la Canada kwa kuwa shirikisho hilo bado halijapata makubaliano ya pamoja ya mazungumzo na timu zake za kitaifa.
Soka la Canada limekuwa chini ya shinikizo kubwa kutoka kwenye timu zake za wanaume na wanawake ikitajwa hasa mzozo wa malipo. Timu ya wanawake ilipanga mgomo mapema mwezi huu lakini ikabadili azama yake kufuatia tishio la kuchukuliwa hatua za kisheria.
Lakini kuna kila dalili ya kususia kambi ya mapema mwezi kesho April ikiwa makubaliano hayajafikiwa. Kuondoka kwa Bontis labda kunaonyesha aina fulani ya maendeleo, kwani hata hivyo timu za wanaume na wanawake ziliomba mabadiliko kwenye uongozi wa soka la Canada.