
Jumatano hii, Rais wa FIFA Gianni Infantino alizindua Uwanja wa Pele jiji Kigali, nchini Rwanda kwa heshima ya nguli wa soka wa Brazil aliyefariki Desemba mwaka jana.
Uwanja huo wa michezo mbalimbali, ambao awali ulijulikana kama Uwanja wa Mkoa wa Kigali, unachukua watu 22,000.
Uzinduzi wa uwanja huo uliofanyika kando ya Kongamano la 73 la Fifa mjini Kigali, uliongozwa na Rais Paul Kagame.
Rais Kagame alimshukuru Bw Infantino kwa kuipa nchi fursa ya kumheshimu Bw Pele kwa kuutaja uwanja huo kwa jina lake, kulingana na gazeti la The News Times.
Bw Infantino alisema hatua hiyo ndiyo njia bora ya kuweka kumbukumbu za soka za Bw Pele.
“Pele alituacha lakini yuko nasi kila wakati,” Bw Infantino alisema.