fbpx

Rais Samia Suluhu atoa pole kuvamiwa kwa kanisa katoliki Geita

Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa Kanisa katoliki nchini kufuatia uvamizi wa Kanisa Kuu la Kiaskofu jimbo la Geita.

Kanisa hilo lililovamiwa usiku wa kuamkia Februari 26 na kuharibiwa vifaa vyote vya uendeshaji wa ibada huku serikali ikiahidi kuchangia ununuzi wa vifaa vipya ili kuwezesha kurejeshwa kwa shughuli za ibada katika kanisa hilo.

Akiongea kwa niaba ya Rais Samia, Mkuu Wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela anasema watahakikisha kufikia tarehe 18 Machi kanisa linaendelea kutoa huduma.

Askofu wa jimbo hilo Mhashamu, Flavian Kasala ameishukuru serikali pamoja na jeshi La Polisi kwa hatua wanazozichukua katika tukio hilo huku akiitaka jamii kuacha kujihusisha na matendo ya kihalifu.

Kamanda Wa Polisi mkoa wa Geita, Safia Jongo anasema jeshi hilo linaendelea na upelelezi ili kupata kiini cha uvamizi na uhalifu Katika kanisa hilo.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights