
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanznia Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza mkutano wa maandalizi ya mkutano wa Afrika wa masuala ya chakula na Kilimo (AGRF) utakaofanyika Septemba 5 hadi 8 Mwaka huu.
Mkutano wa maandalizi ya mkutano huo mkubwa unafanyikia jijini Dar es Salaam ukijumuisha viongozi mbalimbali wa Mataifa ya Afrika hasa sekta za Kilimo na Chakula