fbpx

Polisi yajipanga kukabili uhalifu mitandaoni

Kutokana na ukuaji wa Sayansi na Teknolojia, jeshi la Polisi nchini limekuja na mkakati mpya wa mafunzo yatakayowapa umahili wapelelezi wake ikiwemo matakwa ya kisheria na mambo ya msingi ya kuzingatia katika hatua za awali za upelelezi.

Hayo yamebainishwa na Mkurungezi wa makosa ya jinai nchini, Kamishina wa Polisi, Ramadhan Kingai katika shule ya Polisi Tanzania – CCP iliyopo Moshi Mkoani kilimanjaro wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya kuwapa uwezo na umahiri wapelelezi wa Jeshi la Polisi ikiwemo washiriki kujifunza na kujadili masuala mbalimbali.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights