
Kufuatia tukio la kuvamiwa na kuharibiwa kwa mali katika Kanisa Katoliki jimbo la Geita lililotokea usiku wa kuamkia Februari 26, Jeshi La Polisi mkoa wa Geita limetoa taarifa kuwa mvamizi huyo alifanya tukio akiwa amelewa.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Jeshi La Polisi mkoa wa Geita Safia Jongo na anasema baada ya mahojiano mtuhumiwa huyo amekiri kutekeleza tukio hilo baada ya kulewa sana. Kamanda Jongo alisema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani hivi karibuni.
Kwa upande wake Askofu wa kanisa hilo Mhashamu Flavian Kasala anasema uvamizi huo umesababisha hasara ya zaidi ya shilingi milioni 20