
Zaidi ya theluthi moja ya watu watahitaji misaada ya kibinadamu mwaka huu nchini Sudan kutokana na njaa na ongezeko la idadi ya watu waliokimbia makazi yao katika nchi hiyo ya kaskazini mashariki mwa Afrika mojawapo ya nchi zilizoathiriwa zaidi na njaa duniani.
Idadi ya watu wasio na uhakika wa chakula imeendelea kuongezeka kwa mwaka wa tatu mfululizo.
Watoto milioni nne chini ya miaka mitano na wanawake wajawazito na mama wauguzi ambao watahitaji huduma muhimu kuweza kuishi.
Sudan ni mojawapo ya nchi zilizoathirika zaidi duniani wakati uchumi umedorora tangu mwezi oktoba 2021 na kusitishwa kwa misaada ya kimataifa, takriban watu milioni 15.8 watahitaji msaada wa kibinadamu au milioni 1.5 zaidi ya mwaka 2022 ongezeko kubwa zaidi tangu 2011.
Katika mojawapo ya nchi zilizo hatarini zaidi duniani kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na mafuriko bado yameathiri watu 349,000 mwaka 2022 huku homa ya Dengue na Malaria vikistawi katika maji yaliyotuama.